Uteuzi wa wachezaji watakaowakilisha kaunti ya kilifi katika mashindano ya kitaifa ya Kenya Youth Inter County sports yatakayofanyika kaunti ya Tharaka Nithi mwezi april mwaka huu unaendelea na wikendi ijayo uteuzi huo utafanyika katika eneo bunge la Malindi uwanjani Alaskan, lakini pia eneo bunge la Magarini.
Naftal Owino ambaye afisa mkuu wa michezo na talanta za vijana katika gatuzi la kilifi anasema kwamba uteuzi huo unafanyika katika kila eneo bunge la kaunti ya kilifi kuchagua wachezaji wenye umri wa miaka kati ya 18 na 23 wakatao wakilisha kaunti katika michezo ya soka lakini pia mpira wa wavu.
Kuningana na Naftali ni kwamba mashirikisho ya FKF ndio yatakaohusika pakubwa katika utafutaji wa wachezaji hao mashinani.

