HAALAND AWEKA HISTORIA MANCITY IKIIADHIBU RB LEIPZIG KLABU BINGWA ULAYA

Baada ya mshambuliaji wa Manchester City, Erling Braut Haaland kufunga mabao 5 hapo jana kwenye ushindi wa mabao 7-0, ushindi walioupata Man City dhidi ya RB Leipzing kwenye mchezo wa klabu bingwa Ulaya, mshambuliaji huyo raia wa Norway amekuwa mchezaji wa tatu kufunga mabao 5, kwenye mchezo mmoja wa ligi ya mabingwa Ulaya na anaungana na Lionel Messi raia wa Argentina aliyefanya hivyo mwaka 2012 na Luiz Adriano wa Brazil mwaka 2014.

Halaand pia amefikisha idadi ya Hat-tricks 5 kwenye michuano yote, ikiwa ni hat-trick ya 3 zaidi ya mchezaji yoyote kwenye Ligi kubwa 5 barani Ulaya msimu huu 2022-23.

Na Haaland amekuwa mchezaji wa kwanza wa ligi kuu nchini Uingereza kufunga Hat-trick 5 ndani ya msimu mmoja tangu 2016-17, akiwa amefikia rekodi ya Harry Kane.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *