STEWART MADZAYO AIKOSOA SERIKALI KUU

Seneta wa kaunti ya Kilifi Stewart Madzayo ameikosoa serikali kuu kwa madai ya kushindwa kufanikisha ahadi ambazo ilitoa kwa Wakenya.
Akizungumza katika eneo la Mtwapa kaunti ya Kilifi kwenye mkutano wa Muungano wa Azimio La Umoja One Kenya Madzayo amesema licha ya Rais William Samoei Ruto kuahidi gharama ya maisha itadhibitiwa baada ya kuingia uongozini hakuna mikakati ambayo imewekwa kudhibiti hali hiyo.
Vilevile, Madzayo pamoja na viongozi wengine wa pwani wamelalamikia uteuzi wa Nahodha William Kipkemboi Ruto kuwa mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya usimamizi wa bandari ya Mombasa wakisema nafasi hiyo ilipaswa kukabidhiwa mpwani.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *