WANAWAKE WENYE TABIA YA KUOMBA PESA KWA WANAUME MWISHOWE HUNYANYASWA KINGONO MAKUBALIANO YAKIKIUKWA

Baadhi ya visa vya wanawake kudhulumiwa kingono na wanaume vinadaiwa kuchangiwa na makubaliano baina ya wawili hao kukosa kuafikiwa.
Haya ni kulingana na Mwenyekiti wa shirika la kutetea haki za wanawake na watoto la KILIFI MUMS kaunti ya Kilifi Kibibi Ali ambaye amesema baadhi ya wanawake wamekuwa na tabia za kuomba pesa za mahitaji kutoka kwa wanaume ambao mwishowe hutaka kulipwa kupitia kufanya ngono kulingana na makubaliano yaliyokuwepo baina yao.
Kutokana na hilo baadhi ya wanaume huwa wanaamua kuchukua hatua ya kuwadhulumu wanawake kingono kutokana na kuwa wametumia fedha zao kwao.
Aidha, Kibibi amewataka kutafuta njia mbadala za kutatua mizozo baina yao bila kuchukua sheria mkononi.