TUTACHEZA KADRI YA UWEZO WETU, ASEMA JERGEN KLOPP

Mkufunzi Jergen Klopp anayekiongoza kikosi cha Liverpool amesema kwamba watajaribu uwezo wao kuandikisha historia katika mechi ya usiku wa leo kwenye klabu bingwa ulaya vijana wake watakapokuwa wanachuana na Real Madrid katika dimba la Santiago Bernabou.

Mkufunzi huyo anasema kwamba licha ya kuonekana kwamba tayari huenda wakawa wameagana na mashindano hayo baada ya kipigo cha mabao 5-2 katika mechi ya raundi ya kwanza Anfield amesema kwamba watacheza kwa heshima ya mashindano hayo ila lengo kuu kusajili ushindi.

Mechi nyingine ya klabu bingwa ulaya usiku wa leo ni ile ya Napoli dhidi ya Frankfurt mechi zote zikichezwa mwendo wa saa tano usiku wa leo.