David Ouma ambaye ni mkufunzi wa klabu ya sofapaka anasema anamatumaini makubwa ya kushinda kombe la Mozzert Bet mwaka huu.
Anasema licha ya klabu yake kuyumba katika ligi ya fkf msimu huu vijana hao wa batoto ba mungu wako na uwezo mkubwa wa kungangania taji hilo kwani wanawekeza nguzu sawa katika kila mashindano ili kuibuka na ubingwa.
Mkufunzi huyo anasema kwamba kwa sasa Sofapaka inalenga kufanya usajili wa kutosha ili kuimarisha kikosi chake hasa katika mzunguko wa pili wa ligi kuu ya primia msimu huu.
Ameweka wazi kwamba watafanya usajili wa wachezaji wenye ari na malengo ya mafanikio ili kurudisha heshima katika klabu hiyo ambayo imeshinda mataji takriban yote katika taifa hili.
Katika ligi ya primia Sofapaka inasimama katika nafasi ya 13 na alama 22 kwa kucheza mechi 19 msimu huu.

