ARSENAL YANG’AA KWENYE TUZO ZA LONDON

Mikel Arteta ambaye ni mkufunzi mkuuwa klabu ya Arsenal anasema anaimani ya kushinda ubingwa wa ligi kuu nchini Uingereza msimu huu kutokana na kiwango kizuri viajana wake walichonacho kwa sasa.

Arteta alikuwa akiyazungumza hayo baada ya kupata tuzo la mkufunzi bora wa mwaka katika jiji la London tuzo zilizofanyika jana Jumatatu.

Bukayo saka wa Gunners pia alishinda tuzo la mchezaji bora mchanga, Martin Odeguard akishinda tuzo la mchezaji bora wa mwaka katika tuzo hizo za London na hatimaye mlinda lango wa washika mtutu hao Aaron Ramsdale amejinyakulia tuzo la kipa bora.