Ni rasmi sasa klabu ya Talanta Fc imemsajili Augustine Kuta kutoka klabu ya Matahre United katika mkataba wa muda ambao mpaka sasa haujawekwa wazi.
Kuta ni mmoja tu ya wachezaji ambao wametua FC Talanta katika dirisha hili ingawa kwake kuondoka Mathare United ni kutafuta nafasi zaidi ya kucheza baada ya kukosa nafasi katika kikosi cha kwanza.
Klabu ya Afrika kusini Orlando Pirates inaangalia uwezekano wa kumsajili mshambuliaji wa GoR Mahia mwite Benson Omala.
Omala amekuwa na kiwango kizuri na kikosi cha mkufunzi JohnNathan McKINSTRY Msimu huu na amefunga mabao 19 katika mechi 19 za ligi kuu msimu huu.

