Nahodha wa klabu ya Olympics Pirates mwite Saica Romano amekiri kwamba vilabu vya Malindi kaunti ya Kilifi katika ligi ya daraja la kwanza kitaifa vimeimarika kisoka.
Romano anayasema hayo baada ya klabu yake kutandikwa kichapo cha mabao 4-0 dhidi ya Malindi Progressive katika uwanja wa Alaskan siku ya Jumapili.
Nahodha huyo kutoka kaunti ya Isiolo amesema kwamba viwango vya soka na talanta kaunti ya Kilifi vimeimarika katika siku za hivi punde hivyo kuleta ushindani mkubwa katika ligi za kitaifa.
Nahodha huyo ameongoza kwamba changamoto za usafiri pamoja na hela za kutosha kusaidia wachezaji katika mechi za mbali kutoka Isiolo ndio jambo ambalo linalemaza klabu hiyo licha ya kuwa na kiwango kizuri pia kwenye soka.
Kwa sasa Young Bulls lakini pia Malindi Progressive ndio vilabu vya kaunti ya Kilifi vinavyocheza lifi kuu ya daraja la kwanza kitaifa.

