GAVANA WA LAMU ASEMA NI KUPITIA SERIKALI YA KAUNTI HIYO NDIPO MIZOZO YA ARDHI ITATATULIWA

Gavana wa kaunti ya Lamu Issa Abdalla Timamy amesema ni kupitia serikali ya kaunti hiyo pamoja na bunge la kaunti ya Lamu ndipo suala la mizozo ya ardhi kwenye kaunti hiyo itaweza kupata mwafaka.
Kulingana naTimamy katiba ya nchi, ardhi imegatuliwa na ni vyongozi wa kaunti hiyo ambao wanaweza kushughulikia mizozo hiyo ili wenyeji wapate hatimiliki za ardhi.
Timamy amesema hakuna mtu ambaye ataruhusiwa kuingia katika mashamba ya kibinafsi na kutaka kupewa hatimiliki za ardhi.