Mkufunzi Erick Ten Hag anasema kwamba ni sharti vijana wake wasajili ushindi dhidi ya Liverpool ili vijana wake wasalie katika kinyanganyiro cha kuwania ubingwa wa ligi kuu msimu huu.
The Red Devils watasafiri hadi Anfield siku ya jumapili kuchuana na wekundu wa Mersisyde wanaoongozwa na mkufunzi Jergen Klopp.
Kwa upande wake Klopp anasema ushindi wa katikati ya wiki dhidi ya Wolveshampoton umewapa vijana wake motisha kuelekea wikendi ijayo huku wakilenga kufufua matumaini ya kumaliza nne bora msimu huu.
Mara ya mwisho Man U kucheza dhidi ya Liverpool katika uwanja wa Anfield walipoteza kwa kichapon cha mabao 4-0 katika mechi ya primia.

