TUNASUBIRI TU KANTONGA KESHO, YANGA

Nahodha wa klabu ya Yanga fc Hamisi Najib anasema ako na matumaini makubwa ya kusajili ushindi wa alama tatu kwenye mechi ya kesho dhidi ya Kamtonga fc kutoka Taita Taveta, mechi ambayo itachezwa mjini malindi katika uwanja wa Alaskan.

Hamisi anasema kwamba klabu hiyo ya daraja la pili kitaifa imefanya mazoezi ya kutosha wiki hii katika matayarisho ya mechi ya kesho wakiwa nyumbani kwa kurekebisha makosa ambayo yamekuwa yakiwaponza awali katika mechi za ligi msimu huu.

Nahodha huyo ameambia Tama La Spoti kwamba sare yao dhidi ya Inter Dabaso katika Daby ya kaunti ya Kilifi ilitokana na ukosefu wa matayarisho ya kutosha pamoja na uwanja mbovu wa Inter Dabaso.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *