Jamii kaunti ya Kilifi na eneo la Pwani kwa jumla imetakiwa kutokubali dhumula za aina yoyote katika jamii na badala yake kusisitiza suala la haki na usawa kwa kila mwananchi.
Haya ni kwa mujibu wa afisa wa shirika la AIDS SERVICES KENYA, Betty Mwacheda ambaye amesema wananchi wanapaswa kuhakikisha wanafahamu haki zao kikatiba na kuwashtaki wale wanaotekeleza wanaohusika na visa hivyo.
Vilevile, amewataka wananchi kuwasisitiza viongozi wao kuwatekelezea miradi ya maendeleo katika maeneo yao kwa mujibu wa sheria ili kuwapunguza baadhi ya matatizo yanayowakabili katika kuendeleza shughuli zao katika jamii.
Kwa upande wake Robert Mumba, kiongozi wa vijana katika bunge la Vijana kaunti ya Kilifi, amesema kuwa kama vijana wa kaunti hii ya Kilifi wamejitolea kusaidia jamii, katika juhudi zao za kupata haki dhidi ya masuala mbalimbali ambayo huwakabili wanajamii hao, zikiwemo kesi za dhuluma dhidi yao.
JAMII KAUNTI YA KILIFI YATAKIWA KUKABILI VISA VYA DULUMA ZA KIJAMII

