FRED MATIANG’I ATARAJIWA KUFIKA KATIKA AFISI ZA DCI

Aliyekuwa waziri wa usalama wa ndani, Dkt. Fred Matiangi sasa anatarajiwa kufika katika ofisi za idara ya DCI, kuandikisha taarifa kuhusiana na yaliyojiri mwezi Februari tarehe 8 ambapo kuibuliwa madai kuwa maafisa wa polisi walivamia nyumbani kwake swala lililopingwa na mkuu wa idara ya upelelezi Mohamed Amin.
Hii ni baada ya Matiangi kuwasili nchini baada ya ziara yake ya wiki mbili kule Uingereza.
ujio wa Matiangi umejiri baada ya ati ati kukumba kuonda kwake nchini pindi tu baada ya maafisa wa idara ya uchunguzi kuvamia nyumbani kwake.
Inaarifiwa kuwa ndege ya KLM iliyokuwa imembeba Matiangi ilitua katika uwanja wa ndege wa JKIA usiku wa jumamosi.
Tume ya maadili EACC pia imeandikia waraka baadhi ya vitengo vya serikali ikitaka kupewa fomu za Matiangi zakutangaza mali yake.