MSHINDI WA FKF CUP KUPATA MILIONI 4

Mashindano ya FKF Cup yamepata udhamini baada ya kusainiwa kwa dili la milioni 60 kutoka kwa kampuni ya ubashiri ya Mozzzert Bet.

Shirikisho la soka nchini FKF jana lilisaini mkataba huo wa miaka mitatu ambao unalenga kusimamia masualaya usafiri, upeperushaji wa matangazo ya moja kwa moja pamoja na uchapishaji wa chapa zitakazosaidia mauzo ya mashindano hayo makongwe zaidi ya taifa hili.

Kulingana na naibu rais wa fkf Doris Petra ni kwamba mashindi wa mashindano hayo mwaka huu atakwenda nyumbani na shilingi milioni 4.2 tofauti na awali ambapo mshindi alifaidika na kutwa milioni mbili pekee huku nafasi ya pili akishinda milioni moja.

Wakati hayo yakijiri, Gor Mahia imepigwa breki katika ligi kuu nchini Kenya baada ya kushushiwa kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Mathare United.

Hii ni baada ya kuwa na muendelezo wa matokeo mazuri msimu huu wakicheza mechi 11 bila kupoteza mechi hata moja.

Sasa Gor Mahia maarufu kama Kogalo ambao ni mabingwa mara 19 wa ligi hiyo bado inasalia kuongoza ligi na alama 37 alama nne mbele ya Nzoia sugar ambayo inasimama katika nafasi ya pili.

Kwengine ni kwamba Vihiga Bullets inazidi kuona masaibu ligini baada ya mchana wa leo kushushiwa kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Talanta fc.