Wito umetolewa kwa viongozi wa michezo kuingia mashinani zaidi kutambua na kukuza talanta za vijana katika eneo bunge la Magarini kaunti ya Kilifi.
Akizungumza na Tama la Spoti baada ya mashindano ya soka yaliyokuwa yanatumika kuzindua mradi wa kusambaza injili na shirika la Youth For Christ Kenya mjini marafa katika uwanja wa Polytechnic, mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Shem Irungu amesema kwamba mashinani kuna vijana wengi wenye talanta ambazo zinauwezo wa kuwakilisha taifa iwapo zitatambuliwa na kupewa malezi.
Ni kauli ambayo imeungwa mkono na Nelly Kagoru ambaye ni mkurugenzi wa kituo cha Lulu FM pamoja na shirika linalohusika na masuala ya watoto la Dream of African Child aliyesema kuna umuhimu mkubwa wa kulea vipaji vya vijana hao ili kufikia vilele vya talanta na ndoto zao maishani.

