KWANTHANZE YASHINDA UBINGWA AFRICA

Shule ya upili ya Kwanthanze ndio mabingwa wa mashiondano ya shule za upili afrika nzima katika mashindano ya mpira wa wavu mwaka huu.

Malkia hao kutoka kaunti ya Machakos wamechukua ufanisi huo kwa kuichapa Lycee Bin Anzarane kutoka taifa la Morocco kwa seti tatu bila jawabu na kuhifadhi ubingwa huo wa Afrika.

Kwanzathanze wamekuwa na ufanisi kitaifa,mashindano ya Afrika Mashariki na ni shule ambayo imekuwa ikichangia baadhi ya wachezaji waliojiunga na timu ya taifa ya mpira wa wavu Malkia Strikers.