Mechi ya daraja la pili kitaifa ya Furunzi FC dhidi ya Maji Bombers ililazimika kusitishwa na shirikisho la soka kutokana na klabu ya Maji Bombers kuingia kwenye rekodi mbaya ya kushuka daraja msimu huu.
Hii ni kutokana na klabu hiyo ya eneo bunge la malindi kaunti ya kilifi kukosa kuheshimu ratiba mara tatu mfululizo msimu huu.
Kwa sasa klabu hiyo inasubiri taarifa rasmi kutoka kwa fkf kuhusu kutolewa kwenye ligi hiyo na kushushwa hadi ligi ya mkoa wa pwani.
Maji Bombers imekuwa na kipindi kigumu kutokana na ukata wa kifedha msimu huu jambo lililopelekea baadhi ya wachezaji kujiondoa na kujiunga na vilabu vingine.

