Nahodha wa klabu ya Malindi Progressive mwite Bernard Lusi anasema uchovu wa wachezaji kutokana na changamoto ya usafiri ndio jambo kubwa lililowaponza wikendi ilopita walipopiga sare ya bao 1-1 dhidi ya klabu ya Kibera Soccer jijini Nairobi.
Kulingana na Lusi ni kwamba basi lao walilokuwa wameabiri liliharibika katikati ya safari tukio ambalo liliwafanya kuchelewa kufika Nairobi na wachezaji wakakosa muda murwa wa kupumzika kabla ya mechi.
Lusi ameambia Tama la Spoti pamoja na kutoa hakikisho kwa mashabiki wa klabu hiyo ya malindi kwamba Malindi Progressive inalenga kushinda mechi yao ya wikendi katika dimba la nyumbani Alaskan ambapo watakuwa wanashuka dimbani dhidi ya ya klabu ya Balaji.

