SERIKALI YA KILIFI YALENGA KUANZISHA MASHINDANO YA GOVERNOR’S CUP

Wizara ya michezo na jinsi katika kaunti ya Kilifi inalenga kuanzisha mashindano ya Governors Cup mwaka huu katika lengo la kusaidia na kuinua vipaji vya michezo kwa vijana katika kaunti hii.

Akizungumza na tama la spoti asubui ya leo Ruth Dama masha ambaye ni waziri wa michezo katika kaunti ya kilifi anasema mashindano hayo yanalenga kutumika kuchagua wachezaji kutoka maendeo bunge mablimbali ya kaunti hii ambao watatengeneza timu itakayopewa ufadhili wa michezo.

Mradi huo unalenga kufanya kazi katika kufanikisha mradi wa serikali serikali kuu wa Talanta hela wa kukuza vipaji pamoja na kufanya talanta kuwa ajira.

Kulingana na Ruth ni kwamba serikali imetenga bajeti ya michezo ya kusambaza vifaa vya kuwasaidia wachezaji mashinani kupitia wawakilishi wadi ili kuimarisha michezo ya wachezaji hao hao.