Afisa wa afya ya umma kaunti ndogo ya Changamwe kaunti ya Mombasa, Boniface Mbindyo amesema kuwa idadi ya maambukizi ya virusi vya ukimwi imefikia elfu 39 katika kaunti ndogo hiyo.
Mbindyo amesema kuwa kuna haja ya hamasa kwa umma kuimarishwa kuhusiana na mbinu za kujikinga dhidi ya maambukizi ya virusi vya ukimwi ili kuona kwamba maambukizi mapya hayashuhudiwi kwa wingi.
Aidha Mbindyo amesema uwepo wa dawa za kukabiliana na makali ya virusi hivyo vya ukimwi arv’s umesaidia kupunguza idadi ya vifo vya watu wanaoishi na virusi vya ukimwi.
Mbindyo amewatahadharisha wanajamii eneo hilo kutopuuza mbinu za kujikinga dhidi ya maambukizi ya virusi vya ukimwi sawia na magonjwa ya zinaa kama mbinu mojawapo ya kujilinda kiafya,kauli iliyoungwa mkono na afisa wa nyanjani katika shirika la vijana la stretchers Rebecca Achieng.
MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI VINAENDELEA KUONGEZEKA ENEO LA CHANGAMWE

