Waziri wa michezo, sanaa, tamaduni, jinsia, vijana, michezo na huduma za jamii kaunti ya Kilifi, Dkt. Dama Masha amewataka wazazi katika jamii kujukumika katika kuwakuza wanao kiupande wa vipaji na talanta kama mbinu mojawapo ya kuwaimarisha.
Akizungumza katika mahojiano ya kipekee na Lulu fm, waziri Dama amesema kuwa walimu pia wanajukumu la kuwainua wanafunzi kwa upande wa vipawa mbalimbali ili kuona kwamba swala hilo linafanikishwa.
Waziri Dama amesema kuwa ameweka mikakati ya kuhakikisha vijana kwenye kaunti ndogo zote za kaunti ya Kilifi wanaimarishwa kupitia talanta kwani tayari viongozi wa mashinani wamepewa wajibu wa kuunda kamati za mashinani za kutambua talanta za sanaa na michezo miongoni mwa vijana mashinani.
Waziri Dama amesema kuwa wanaweka juhudi za kuboresha viwanja vya michezo mbalimbali kama soka na mpira wa vikapu akiahidi kuwa kufikia mwezi wanne mwaka huu viwanja hivyo vitakuwa tayari
WAZAZI KAUNTI YA KILIFI WATAKIWA KUKUZA VIPAJI NA TALANTA ZA WATOTO WAO

