WAZIRI DAMA MASHA ASEMA WATAKABILIANA NA ONGEZEKO LA DHULUMA ZA KIJINSIA MIONGONI MWA WENYEJI WA KILIFI

Waziri wa michezo, tamaduni, sanaa na jinsia kaunti ya Kilifi Dkt. Dama Masha amesema wizara hiyo inalenga kukabiliana na ongezeko la dhulma za kijinsia miongoni mwa wanajamii kaunti ya Kilifi.

Akizungumza kwenye mahojiano ya kipekee hapa Lulu fm, waziri Dama amesema akina mama, watoto na hata wazee ni miongoni mwa wanajamii wanaopitia dhulma nyingi katika kaunti ya Kilifi.

Dama amesema licha ya kuwa wanaendeleza mikakati ya kukabiliana na dhulma za kijinsia utafiti umebaini kuwa dhulma za kijinsia katika kaunti ya Kilifi zimepungua ikilinganishwa na hapo awali.

Wakati uo huo Waziri huyo ameitaka jamii na wadau mbalimbali kushirikiana katika kupiga vita dhidi ya dhulma za kijinsia katika kaunti hii ya KILIFI.