klabu ya soka ya Kamtonga Fc kutoka eneo bunge la Mwatate kaunti ya Taita Taveta sasa ina malengo ya kutimba katika ligi ya daraja la kwanza kitaifa mwaka ujao baada ya kuimarika kwa matokeo yake kwenye ligi ya daraja la pili kitaifa.
Kulingana na meneja wa kiufundi wa Kantonga mwite Gedion Ndambuki ni kwamba sasa wanafanya kila jitihada kuhakikisha wanaibuka kileleni mwishoni mwa msimu huu.
Wikendi ilopita Kantonga walizawadiwa ushindi wa mabao 2-0 na alama tatu kutokana na wageni wao Beach Bay kutoka Magarini kukosa kuheshimu ratiba kutokana na ukosefu wa usafiri.
Ndambuki akiongeza kwamba tayari wamefanya usajili wa wachezaji ambao wamejiunga na kikosi chake.

