GUARDIOLA YWAMUOMBA RADHI GERARD

Mkufunzi wa klabu ya Manchester City, Pep Guardiola hadharani amemuomba radhi Steven Gerrad kwa kauli aliyoitoa hivi majuzi ya kumkejeli nyota huyo ambaye ni nahodha wa zamani wa klabu ya Liverpool alipomdharau kwa kauli ya kusema Mancheter City ndio chanzo cha Gerard kuteleza na kuanguka.

Tukio linasalia katika historia ya soka ya ligi kuu nchini Uingereza kwa kuikosesha ubingwa wa ligi Liverpool na Manchester City kushinda ubingwa wake wa pili mwaka 2014.

Guardiola akizungumza na wanahabari ameomba radhi kwa Gerrard akisema anajutia kwa kutoa kauli hiyo ya kijinga, kumsuta mchezaji ambaye ako na mchango mkubwa katika ligi kuu ya uingereza pamoja na timu ya taifa ya the Three Lions.