Miamba wa Ujerumani waite Bayern Munich usiku wa kuamkia leo wamesajili suhindi wa bao 1-0 dhidi ya Paris Saint Germain katika dimba la ugenini la Parc De Princes.
Bao la pekee na la ushindi kwenye mechi hiyo lilifungwa na Kingsley Coman katika dakika ya 53, akitendea haki pasi nyerezi iliyotoka kwa beki wa kupanda na kushuka Alphonso Davis.
Katika dimba lingine ni kwamba Tottenham Hotspers ya mkufunzi Antonio Conte imekubali kipigo cha ugenini cha bao 1-0 dhidi ya Ac Milan katika uwanja wa kihistoria San Ciro.
Kiungo Brahim Diaz katika dakika ya saba ya mchezo huyo ndiye aliyefunga bao lililoipa AC Milan ambao ni mabingwa mara 7 wa mashindano haya faida ya nyumbani.
Mechi za marudiano zimeratibiwa kuchezwa mwezi machi tarehe 8 na 9.

