Mkufunzi wa klabu ya Yanga Collins Omol kutoka mjini Malindi kaunti ya Kilifi, klabu inayocheza daraja la pili kitaifa anasema ugumu wa usafiri unasalia kuwa changamoto kubwa katika klabu yake kwa sasa jambo ambalo liliiponza Yanga katika mechi ya ugenini wikendi ilopita mjini Mombasa ambako walipoiga sare ya bao 1-1 dhidi ya klabu ya Ashton Rangers.
Omol akizungumza na Tama La Spoti jioni ya leo katika uwanja wao wa mazoezi mjini Malindi katika shule ya msingi ya Central anasema kwamba uchovu wa safari iliyokuwa na changamoto nyingi uliwalemaza vijana wake ndiposa wakapata sare hiyo.
Mkufunzi Omol hata hiyo amesema kwamba ako na matumaini makubwa ya kusajili ushindi wikendi ijayo dhidi ya klabu ya Shimanzi wakati vijana wake watakuwa nyumbani. Hii ni kutokana na mazoezi ambayo wanafanya katika maandalizi ya mtanangwe huo.

