HURIA YAANDAA MAONYESHO YA UTAMADUNI KWENYE UKUMBI WA TONONOKA

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la kutetea haki za kibinadamu la HURIA Yusuf Lule amesema maomyesho ya utamaduni ambayo yaliandaliwa jana kwenye ukumbi wa Tononoka kaunti ya Mombasa na kuwaleta pamoja wanawake wa jamii mablimbali yalipania kuhamasisha dhidi ya dhuluma za kijinsia.
Kulingana na Lule wanashirikiana na shirika la SEARCH FOR COMMON GROUND kuhamasisha wanawake wa kanda ya pwani namna ya kudhibiti dhuluma hizo.
Amesema ushawishi wa kina mama pamoja na viongozi wa kike utasaidia katika kudhibiti visa hivyo kwenye jamii.
Naye Betty Sidi ambaye ni afisa mkuu wa mradi katika shirika hilo amesema utachangia kufanikisha umoja na uwiano miongoni mwa wanawake kutoka jamii mbalimbali kaunti ya Mombasa kwa ajili ya kuimarisha amani na maendeleo kwenye kaunti hiyo.
Kwa upande wake afisa wa shirika la UJAMAA CENTER kaunti ya Mombasa Grace Oloo amesema mbinu hiyo itasaidia katika kufanikisha mchakato wa kuunganisha jamii.