VISA VYA WASICHANA KUACHA MASOMO KUTOKANA NA UJAUZITO VINAENDELEA KUKITHIRI TAITA TAVETA

Kamanda wa polisi kaunti ya Kwale Josphat Kinyua amesema visa vya wasichana kuacha masomo kufuatia ujauzito vinazidi kukithiri katika maeneo mengi ya kaunti hiyo.
Kinyua amesema visa hivyo vinachangia kwa ongezeko la umaskini katika jamii huku akiwataka wanajamii kupatia elimu kipaumbele.
Kufuatia hilo, kamanda huyo pamoja na wakuu wengine wa usalama wamesisitiza haja ya jamii kuwaruhusu wasichana waliocha shule kufuatia ujazito warejee shuleni ili wajiendeleze kimasomo.
Kinyua amesema kuwa shinikizo za kupatia elimu kipaumbele ni kutokana na swala kuwa hiyo ni mojawapo wa mbinu ya kujikwamua kwenye umaskini uliokithiri.