Gavana wa kaunti ya Kwale Fatuma Achani amesema wanafunzi ambao watapata ufadhili wa masomo ya shule za upili ni wa kaunti hiyo.
Akizungumza akiwa mjini Kwale amewataka wenyeji wa kaunti hiyo kutoingiza siasa kwenye ugavi wa fedha za basari kwa wanafunzi ambao sio wa kaunti hiyo na kusema huenda hilo likachangia kwa wao kukosa kufanya vyema kwenye masomo yao.
Gavana huyo amepuzilia mbali madai ambayo yamekuwa yakiibuliwa kuwa serikali ya kaunti ya Kwale imekuwa ikipeana fedha za basari kiubaguzi na kusema uteuzi wa wanafunzi wenye uhitaji wa karo unatekelezwa na kamati maalumu ili zoezi hili litekelezwa kwa usawa.
GAVANA ACHANI APUUZA MADAI KUWA SERIKALI YA KWALE INAPEANA BASARI KIUBAGUZI

