MANCHESTER UNITED KUUZA WACHEZAJI WATATU NA KUMNUNUA HARRY KANE

Klabu ya Manchester United inalenga kuwauza wachezaji watatu katika dirisha la uhamisho lijalo ili kuangalia uwezekano wa kumnunua Harry Kane mchezaji wa Totenham Hotspurs.

Baadhi ya wachezaji ambao huenda wakauzwa klabuni hapo ni pamoja na beki Harry Maguire, Alex Telles lakini pia fowadi wa timu ya taifa ya Ufaransa Antony Martial mwenye umri wa miaka 27.

Hata hivyo iwapo Manchester United watawaza kuwasilisha ombi tena la kutaka kumnunua Declan Rice kutoka WestHam United watalazimika kutumia pauni milioni 120 kumnasa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24 baada ya ombi lao la kwanza la pauni milioni 100 la mwezi January kukataliwa.

Fowadi wa klabu ya Atson Villa mwite Felipe Coutinho amekataa ofa ya kuondoka Villa Park na kujiunga na klabu ya Galatasary. Mchezaji huyo wa brazil mwnye umri wa miaka 30 amekosa kuwa na kiwango kizuri chini ya mkufunzi wake mpya Unai Emery na sasa amekuwa akiangalia uwezekano wa kujiunga na klabu nyingine.