Klabu ya APS Bomet imepigwa marufuku ya kushiriki mechi za National Super League za msimu wa mwaka 2022/2023 lakini pia wameshushwa daraja hadi ligi ya daraja la kwanza kitaifa kwa msimu ujao wa 2023/2024 kutokana nao kukosa kuheshimu ratiba za mechi.
Kulingana na shirikisho la soka FKF ni kwamba APS Bomet wamekosa kuandikia shirikisho hilo waraka rasmi na sababu maalumu za kukosa kuheshimu ratiba za mechi kwa mujibu wa sheria za shirikisho.
Hadi kufikia sasa APS Bomet wamekosa kuheshimu ratiba katika mechi tatu mfululizo wakisubiri uamuzi wa kesi waliowasilisha mahakamani awali wakitaka kusalia katika ligi kuu ya fkf kutokana na kwamba msimu uliopita walimaliza ligi katika nafasi ya kwanza kwenye NSL.

