TUNAIMANI VIONGOZI WA SASA WATAIMARISHA MICHEZO YA KILIFI – ELLY KATANA

Wadau wa michezo katika kaunti ya Kilifi wameeleza imani yao kwa uongozi wa sasa wa kaunti hiyo wakisema kwamba kuna matumaini michezo huenda ikasonga mbele.

Elly Katana ambaye ni mkufunzi mkuu wa kikosi cha Malindi Progressive FC na anasema kwamba michezo ya kaunti hii huenda ikaanza kuinuka kutokana na  viongozi wa serikali  walichaguliwa kuhudumu katika nyadhfa mbali mbali kwa sasa wameonyesha nia ya kuinua michezo ya vijana.

Mkufunzi huyo ametoa wito kwa viongozi wa kaunti kuwekeza zaidi katika michezo kwa kujenga viwanja vya kisasa ambavyo vitasaidia katika makuzi ya talanta na michezo mbali mbali Kilifi.