TUTASHINDA DABI YA KILIFI – PETER MOLE

Mkufunzi mkuu wa klabu ya Beach Bay Peter Mole anasema kwamba ana matumaini makubwa ya kushinda dabi ya kaunti ya Kilifi ya wikendi ijayo vijana wake watakapokuwa wanashuka dimbani dhidi ya Furunzi FC ugenini katika dimba la Alaskan.

Licha ya kuwa na msururu wa matokeo mabaya msimu huu wa mwaka 2022/2023,  Peter Mole amesema kwamba wako tayari kurekebisha makosa ya awali pamoja na kwamba wiki hii wamekuwa wakipiga tizi za kutosha kujiimarisha kwa dabi hiyo siku ya Jumapili (29-01-2023).

Hadi kufikia sasa Beach Bay wameshinda mechi moja pekee msimu huu, na wamepiga sare mara moja na kutandikwa mara mbili.