TUNALENGA NSL – GAUCHO

Mkufunzi mkuu wa klabu ya Young Bulls maarufu kama Gaucho anasema kwamba matumaini yapo kwa klabu hiyo kupanda daraja msimu ujao hadi National Super League.

Gaucho anazungumza hayo baada ya kuitandika mahasimu wao mjini Malindi, , klabu ya Malindi Progressive kichapo cha mabao 2-1 wikendi ilopita katika uwanja wa shule ya upili ya wavulana Malindi.

Amesema kwa sasa wanalenga kupanda daraja baada ya kucheza ligi hiyo kwa kipindi cha misimu mitatu mfululizo.

Mkufunzi huyo anasema kwamba kwa sasa wanafanya mabadiliko katika kikosi chake kupitia usajili jambo ambalo anamatumaini litasaidia kupatia klabu hiyo kasi na kuimarika zaidi katika msimu huu wa 2022/2023.