VURUGU MICHEZONI NI TISHIO KWA MADHAMINI MAGARINI

Naibu mwenyekiti wa shirikisho la soka eneo bunge la Magarini kaunti ya Kilifi mwite Katana Shilingi anasema utovu wa nidhamu miongoni mwa mashabiki lakini pia wachezaji ni changamoto kubwa inayokumba sekta hiyo mashinani.

Kiongozi huyo amehoji kuwa uwepo wa vurugu la mara kwa mara wakati wa mechi unafukuza wadhamini ambao huenda wangesaidia katika makuzi ya talanta za wachezaji.

Katana amekiri kwamba mbali na changamoto nyingine zinazokumba soka la mashinani uongozi wa mchezo huo Magarini umeanza kuhamasisha umma kuhusu kudumisha nidhamu wakati wa mashindano.