WEKEZENI MICHEZONI, ABABU ASHAURI KAUNTI

Waziri wa michezo Ababu Namwamba ameshauri serikali za kaunti kuwekeza zaidi katika miundo mbinu ya kuwezesha michezo katika kaunti zao.

Amesema ipo haja ya kaunti kutenga pesa za kutengeneza viwanja vya kisasa ili kusaidia malezi ya talanta mbali mbali hapa nchini huku taifa la Kenya likilenga kutuma ombi kwa shirikisho la soka barani Afrika CAF, ombi la kutaka Kenya ipewe nafasi ya kuandaa mashindano ya soka ya kombela afcon mwaka 2027.

Amesema serikali za kaunti zinajukumu kubwa la kuanzisha miradi ya michezo itakayovutia wawekezaji binafsi ambao huenda wakajitokeza na kusaidia kuimarika kwa sekta hiyo.

Alikuwa akiyasema hayo wakati wa ufunguzi wa mashindano ya michezo na utamaduni katika kaunti ya Kisumu uwanjani Jomo Kenyatta.