VIONGOZI WA KILIFI WASHAURIWA KUJENGA VIWANJA

Mkufunzi mkuu wa klabu ya Malindi Progressive Elly Katana  anasema ukosefu wa viwanja katika kaunti ya Kilifi ni changamoto kubwa inayokumba sekta ya michezo.

Akizungumza na Tama La spoti  mjini malindi Elly Katana amehoji kwamba kwa sasa viwanja vingi vinamilikiwa na watu binafsi jambo ambalo linakatisha tamaa wachezaji pindi tu wamiliki wa viwanja hivyo wanapovichukua.

Mkufunzi huyo ameshauri viongozi wa kaunti hii kuwekeza zaidi katika ujenzi wa viwanja ili kusaidia vijana kukuza talanta zao.