Mwekahazina wa shirikisho la soka la FKF tawi la eneo bunge la Malindi Jonson Mwabati amehakikishia vilabu vya mashinani kwamba masimu mpya wa ligi hiyo utaanza rasmi mwishoni mwa mwezi huu wa Januari.
Akizungumza na tama la spoti jana katika uwanja wa shule ya upili ya wavulana ya Malindi alisema kwamba kwa sasa vilabu vingi vya mashinanai vinaendelea na usajili wa ligi hiyo kuona kwamba vilabu vingi vinapewa nafasi ya kushiriki katika ligi za mashinani.
Hata hivyo Mwabati amesisitiza kwamba vilabu hivyo vya mashinani vinafaa kufanya jitihada ya kufanya malipo katika muda unaotakikana ili kukamilisha usajili lakini pia kusaidia kuendesha ligi kwa ubora zaidi.
Amekiri kwamba vilabu vingi kwa sasa vinapitia halingumu kifedha jambo ambalo limechelewesha zoezi la usajili wa mapema.

