MASHABIKI WA MALINDI WAMEANZA KUSTAARABIKA – BERNARD LUSI

Nahodha wa klabu ya Malindi Progressive Bernard Lusi ameeleza kufurahishwa na mashabiki wa malindi kwa kuonyesha ustaarabu kwenye mechi kwa sasa tofauti na zamani ambapo katika mechi za dabi za eneo bunge la malindi kumekuwa kukishuhudiwa vurugu.

Alikuwa akiyasema hayo baada ya mechi ya jana ambapo Malindi Progressive walipoteza kwa kichapo cha mabao 2-1 ugenini katika mechi ya daraja la kwanza kitaifa  dhidi ya mahasimu wao wa kaunti ya Kilifi Young Bulls katika uwanja wa shule ya Upili ya wavulana ya malindi.

Lusi anasema kwa sasa taharuki ya kucheza au hata kushuhudia mechi za dabi hizo imepungua jambo ambalo huenda likachangia mashabiki wengi kujitokeza viwanjani katika siku za usoni.