MESSI NA MBAPPE WAORODHESHWA KATIKA TUZO YA MCHEZAJI BORA WA MWAKA WA FIFA

Bingwa wa mashindano ya kombe la dunia Lionel Messi pamoja na mwenzake wa Paris SG Kylian Mbappe wamewekwa katika orodha washindani wa tuzo la mchezaji bora wa mwaka 2022 na shirikisho la soka duniani fifa.

Messi ambaye ashawahi shinda tuzo hiyo awali, mwaka jana aliisaidia timu yake ya argentina kuwania ubingwa wa kombe la dunia  nchini Qatar ushindi ambao unamwka katika nafasi nzuri ya kujishindia tuzo la nane la Ballon ‘Or lakini pia tuzo hii ya mchezaji bora mwaka 2022.

Wachezaji wangine waliowekwa katika orodha hiyo kutoka klabu ya Paris SG ni pamoja na Neymar Jr wa Brazil pamoja na Ashraf Hakimi beki ambaye aliisaidia Morocco kumaliza nafasi ya nne katika mashindano hayo.