ABABU NAMWAMBA AMUAGIZA MKAGUZI MKUU KUFANYA UCHUNGUZI WA MIRADI

Mkaguzi mkuu wa wizara ya michezo katika serikali kuu Nancy Gathungu amemhakikishia waziri Ababu Namwamba kwamba atatimiza agizo lake ya kufanya uchunguzi kuhusu miradi mbali mbali iliyofeli licha ya hela ndefu kuwekezwa na serikali katika miaka mitano iliyopita.

Haya yanajiri baada ya waziri namwamba kutembelea miradi mbali mbali ambayo kulingana na taarifa walizonazo kuliwekzwa hela nyingi ila huenda zilifujwa. Ametaja kuwa hali ya viwanja nchini Kenya inatamausha jambo ambalo linatishia kuimarika kwa michezo nchini Kenya.

Waziri Namwamba alipochukua nafasi ya kuongoza Wizara ya michezo aliahidi kupiga vita ufisadi ili kusafisha sekta hiyo.