Martin Odegaard kiungo anayechezea klabu ya Arsenal amewapiku nyota wanane wa ligi kuu nchini uingereza na kushinda tuzo ya mchezaji bora mwezi November na December mwaka jana.
Odegaard alishinda kura nyingi za mashabiki na kushinda tuzo hiyo baada ya kufunga mabao 3 na kusaidia ufungaji wa mabao 3 yaliosaidia Arsenal kufanya vyema katika ligi kuu nchini Uingereza.
Raia huyo wa Norwey anakuwa mchezaji wa kwanza wa The Gunners kushina tuzo hiyo baada ya Pierr Aubameyang kufanya hivyo mwaka 2019
Mkufunzi wake Mikel Arteta naye ameshinda tuzo ya mkufunzi bora wa mwezi December baada ya kuiwa na mwendelezo wa matokeo mazuri na kuifanya Arsenal kuongoza ligi katika kipindi hicho.

