Klabu ya Progressive Academy inazidisha mazoezi yake kujiimarisha kwa mechi ya wikendi ambapo watakuwa wanavaana na mahasimu wao Young Bulls katika dadi ya kaunti ya Kilifi ambayo imeratibiwa kurindimwa siku ya jumapili katika dimba la shule ya upili ya wavulana ya Malindi.
Akizungumza na Tama la spoti mapema leo baada ya mazoezi uwanjani Alaskan Bernard Lusi ambaye ni Nahodha wa klabu hiyo anasema timu yake inazidi kujinoa kwa ajili ya pambano hilo.
Progressive Academy ambayo inaongoza ligi ya daraja la kwanza kitaifa na alama 10 baada ya mechi nne inazidi kukomaa katika ligi hiyo huku nahodha Bernanrd Lusi akihoji kwamba motisha unaotokana na malipo mazuri pamoja na urahisishwaji wa shughuli za michezo katika klabu hiyo ndio jambo ambalo linalochangia matokeo hayo mazuri.
Aidha nahodha huyo amemshukuru sana mwakilishi wadi wa mji wa malindi bwana Rashid Odhiambo kwa kuisaidia klabu hiyo kwa miaka mingi jambo ambalo limechangia sana ufanisi wao

