KARIM MANDONGA KUSHIRIKI KATIKA PAMBANO LA KWANZA MAARUFU KENYA

Bondia maarufu kutoka taifa jirani la Tanzania mwite Karim Mandonga ameeleza matumaini yake kwamba atapokelewa kwa heshima kuu na rais wa taifa la Kenya William Samoei Ruto atakaposhuka katika uwanja wa ndege.

Mandonga anatarajiwa kushuka ulingoni dhidi ya bondia Daniel Wanyonyi katika ukumbi wa KICC Tsavo Ballroom mjini Nairobi wikendi ijayo siku ya Jumamosi tarehe 14.

Bondia huyo ameahidi mashabiki wake Tanzania matokeo mazuri katika pambano hilo ambalo ni la kwanza na maarufu  kabisa nchini Kenya katika siku za hivi punde.