Jumla ya shilingi milioni 5 zimetengwa katika bajeti ya ziada kwenye bunge la kaunti ya Kilifi, ili kufadhili masomo ya wanafunzi katika wadi mbalimbali za kaunti ya Kilifi.
Haya ni kulingana na mwakilishi wa wadi ya Ganda eneo bunge la Malindi kaunti ya Kilifi, Oscar Wanje ambaye amesema ugavi wa fedha hizo kwa wanafunzi wenye uhitaji, unatarajiwa kuanza hivi karibuni wakati shule zitakapofunguliwa.
Aidha, amesema wanakamati wa shughuli za ugavi wa fedha hizo za basari katika kila wadi, ndio watakaokuwa na jukumu la kutambua wale wanaostahili kupata ufadhili huo.
Kwa upande wake Sammy Kazungu ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya CDF katika afisi ya mbunge wa Malindi, Amina Mnyazi amesema masuala ya elimu hugharimu fedha nyingi zaidi katika bajeti ya NG-CDF, licha ya wao kuwa na majukumu mengine mengi zaidi kama serikali ya kitaifa.
SHILINGI MILIONI 5 ZATENGWA KATIKA BAJETI YA ZIADA KWENYE BUNGE LA KAUNTI YA KILIFI

