NJAA YAIPONZA BEACH BAY MOMBASA

Mkufunzi mkuu wa klabu ya Beach Bay Peter Mole iliyopoteza mechi yao jana dhidi ya kishada FC, kichapo cha mabao 6-1 mjini Mombasa amelalamikia ukata wa kifedha katika klabu yake kama changamoto kuu iliyochangia matokeo hayo mabovu.

Kulingana na Mole ni kuwa wachezaji wake walisafiri na kucheza wakiwa na njaa pamoja na changamoto ya usafiri jambo ambalo lilichangia wachezaji kukosa motisha wa kusajili matokeo mazuri. Mkufunzi huyo amehoji kwamba walicheza tu kuheshimu ratiba.

Mwalimu huyo wa soka ameshauri uongozi wa eneo bunge la Magharini kuwekeza sana katika michezo ili uimarisha sekta hiyo na kufanya vijana kunoa vipaji vyao kupitia michezo pamoja na kuwaepusha na maovu kama mimba za mapema na kupotea kwa mihadarati.