TUSKER FC YAPEWA KICHAPO NA BANDARI FC MOMBASA

Wanamvinyo Tusker FC wamepoteza mechi yao ya kwanza kabisa katika ligi kuu ya fkf Primia msimu huu baada ya jana kutandikwa kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya wanamaji Bandari fc.

Kabla ya mechi hiyo Tusker walikuwa wameshinda mechi zao zote sita za ligi msimu huu na bado wanaongoza ligi wakiwa na alama 18.

Mabao ya Bandari yalifungwa na Umar Kasumba raia wa Uganda katika dakika ya 9 kabla ya Andrew Juma kugongelea msumari moto kwa ushindi huo kupitia bao lake tamu katika dakika ya 30.

Kwa upande wa wanamvinyo Tusker inayoongozwa na mkufunzi Robert Matano bao la kufutia machozi lilitiwa kimyani na Jackson Macharia katika dakika ya 50.