KAMISHA WA MOMBASA AWATAKA WAZAZI KUWAPELEKA SHULE WATOTO WAO WALIOMALIZA DARASA LA 8

Kamishna wa kaunti ya Mombasa John Otieno amewataka wazazi kuhakikisha kuwa wanawapeleka shule watoto wao waliomaliza darasa la nane ili kufanikisha mpango wa serikali wa asilimia mia moja ya wanafunzi wajiunge na shule za upili.
Otieno amesema kuwa elimu ni muhimu sana katika kuhakikisha kuwa vijana wanaepushwa na kujiunga na magenge ya kihalifu.
Aidha Otieno amewataka wazazi kuwajibika katika malezi huku akiwataka kukoma kuwaficha watoto hao ambao wanatekeleza uhalifu iwapo wanatarajia hali ya usalama kuimarika kwenye maeneo yao.