Rais wa muungano wa riadha duniani Sebatian Coe yupo nchini Kenya kwa sasa baada ya kuwasili hapo jana kwa ziara ambapo analenga kufanya vikao na kamati ya riadha nchini Kenya Nock pamoja na waziri wa michezo Ababu Namwamba kwa lengo kuona jinsi gani riadha za Kenya zitaendeshwa kwa ubora zaidi.
Rais huyo katika siku za hivi punde amesikika sana akisema analenga kusaidiana na uongozi wa fani hiyo nchini Kenya katika vida dhidi ya matumizi ya dawa za kututumua misuli.
Sebastian Coe ameeleza kuridhishwa kwake na taifa la Kenya kusema kwamba watawekeza hela zaidi katika kuwezesha vita hivyo ili hatimaye taifa la Kenya lirudishe imani kwa ulimwengu kwamba riadha sasa zitakuwa zinafanyika kwa uadilifu zaidi.
Mwaka jana Kenya ilikuwa kati ya mataifa ambayo yalikuwa karibu kupigwa marufuku na muungano wa riadha kutoshiriki mashindano ya kimataifa kutokana na idadi kubwa ya wanariadha wa taifa hili ambao wamekuwa wakitumia dawa haramu katika mashindano yao licha ya kwamba baadhi yao tayari wameadhibiwa vilivyo.

